Pata taarifa kuu
CECAFA-ZANZIBAR-ETHIOPIA-SOKA

CECAFA yazichukulia hatua kali Zanzibar na Ethiopia

Baraza la mchezo wa soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA, limeifungia Zanzibar na Ethiopa na kuzitoa faini kwa kuwahusika wachezaji wenye umri mkubwa katika mashindano ya vijana wasiozidi miaka 17 inayoendelea nchini Burundi.

Wachezaji wa Harambee Stars wakishangilia baada ya ushindi wa taji CECAFA.
Wachezaji wa Harambee Stars wakishangilia baada ya ushindi wa taji CECAFA. Goal.com
Matangazo ya kibiashara

Baada ya uchunguzi wa CECAFA, imebainika kuwa Zanzibar ilikuwa na wachezaji wenye umri mkubwa, kinyume na kanuni za CECAFA.

Wachezaji waliotakiwa kushiriki katika michezo hii, ni wale waliozaliwa baada ya mwaka 2002.

Ethipoa nayo imejipata katika hilo baada ya kuwa na wachezaji watatu waliokuwa na umri mkubwa.

Zanzibar, inarejea nyumbani na inatakiwa kulipa fainali ya Dola 15,000 fedha ambazo zilitumiwa kununua tiketi ya ndege lakini kugharamia mahitaji mengine nchini Burundi na wataruhusiwa kushiriki katika mashindano ya CECAFA hadi watakapolipa fedha hizo.

Kwa upande wa Ethiopia, wachezaji waliobainika kuwa na umri mkubwa wamerejeshwa nyumbani na shirikisho kutakiwa kulipa Dola 5,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.