Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Kundi la Islamic State (IS) ladai kuhusika na mashambulizi nchini Sri Lanka bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi (Amaq)
Michezo

Kenya yatawala mbio za Mita 3000 kuruka viunzi na maji

media Kutoka Kushoto: Mshindi wa medali ya Shaba Amos Kirui, mshindi wa medali ya dhahabu Conseslus Kipruto na mshindi wa medali ya fedha Abraham Kibiwott wakisherehekea baada ya kushinda mbio za Mita 3000 kuvuka viunzi na maji katika Uwanja wa Carrara katika ADRIAN DENNIS | AFP

Kenya imeshinda mbio za Mita 3,000 kuvuka viunzi na maji kwa upande wa wanaume katika mashindano ya Jumuiya ya Madola inayoendelea nchini Australia.

Kihistoria, Kenya imekuwa ikitawala mbio hizi. Bingwa wa Olimpiki katika mbio hizi Conseslus Kipruto, aliwaongoza wenzake watatu kunyakua medali ya dhahabu, fedha na shaba.

Kipruto aliibuka mshindi kwa muda wa dakika 8 sekunde 10 nukta 08 akifuatwa na Abraham Kibiwott aliyemaliza kwa muda wa 8:10.62.

Medali ya shaba imemwendea Amos Kirui aliyemaliza kwa muda wa 8:12.62.

Baada ya ushindi huo, Kipruto amesema alitaka Wakenya wenzake kuchukua nafasi ya pili na ya tatu na hivyo aliendelea kuwahimiza.

“Sikutaka kuwaacha wenzangu nyuma, ili washindwe,” alisema.

“Niliwahimiza twende pamoja na nilipoona wamechoka, nikaamua kumalizia,” aliongeza.

Ushindi huu umeiongozea Kenya medali katika jedwali ikiwa na medali mbili za dhababu baada ya kushinda mbio za Mita 800 siku ya Alhamisi.

Matokeo kamili:-

1. Conseslus Kipruto (Kenya) 8:10.08

2. Abraham Kibiwott (Kenya) 8:10.62

3. Amos Kirui (Kenya) 8:12.62

4. Matthew Hughes (Canada) 8:12.33

5. Albert Chemutai (Uganda) 8:19.89 (PB)

6. Jonathan Hopkins (Wales) 8:34.12

7. Ieuan Thomas (Wales) 8:40.02

8. Adam Kirk-Smith (Ireland Kaskazini) 8:48.40

9. James Nipperess (Australia) 8:58.16

10. Simon Charley (Vanuatu) 10:03.08

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana