Pata taarifa kuu
JAMAIKA-AUSTRALIA-MICHEZO

Usain Bolt: Nasikitishwa na nafasi aliyoipata Yohan Blake

Mwanariadha mstaafu na bingwa wa mbio za Mita 100 anayeshikilia rekodi ya dunia Mjamaika Usain Bolt amesema, mwanariadha Yohan Blake aliyewakilisha nchi yake katika mbio za Mita 100 katika michezo ya Jumuiya ya Madola inayoendelea nchini Australia, hajafanya vizuri kwa kutetea Jamaika. 

Mwanariadha mstaafu na bingwa wa mbio za Mita 100 anayeshikilia rekodi ya dunia Mjamaica Usain Bolt (juu kushoto) katika Michezo ya Olimpiki ya 2012akiwa pamoja na Yohan Blake (chini kushoto), Nesta Carter (juu kulia) na Michael Pande (chini kulia).
Mwanariadha mstaafu na bingwa wa mbio za Mita 100 anayeshikilia rekodi ya dunia Mjamaica Usain Bolt (juu kushoto) katika Michezo ya Olimpiki ya 2012akiwa pamoja na Yohan Blake (chini kushoto), Nesta Carter (juu kulia) na Michael Pande (chini kulia). REUTERS/Phil Noble
Matangazo ya kibiashara

Usain Bolt amesema Yohan Blake alikumbwa na wasiwasi uliomfanya kumaliza katika nafasi ya tatu na kushindwa kunyakua medali ya dhahabu.

Bolt ambaye yupo Australia kushuhudia michezo hiyo akiwa Balozi wa riadha, amesema atazungumza na Blake na kumtua moyo lakini pia kumtania.

Mwanaridha huyo wa zamani ameongeza kuwa ni hatari sana kwa mwanaridha kuanza vibaya na baadaye kukumbwa na wasiwasi kama alivyofanya Blake ambaye Bolt, anataka awe kama yeye ili kushinda dhahabu katika mbio za Mita 100 na 200.

Mshindi wa mbio za Mita 100, katika mashindano haya ni Akani Simbine, kutoka Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.