Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Kundi la Islamic State (IS) ladai kuhusika na mashambulizi nchini Sri Lanka bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi (Amaq)
Michezo

Brigedia mstaafu Semakana achaguliwa kuwa rais wa FERWAFA

media Makao makuu ya shirikisho la Soka nchini Rwanda, Ferwafa.

Brigadia mstaafu wa Jeshi la Rwanda Semakana Jean Danascene amechaguliwa kuwa rais wa Shirikisho la soka nchini Rwanda (FERWAFA) katika uchaguzi uliofanyika jana mjini Kigali.

Semakana mwenye umri wa miaka 60 alipata kura 45 dhidi ya saba alizopata mpinzani wake Luis Rurangirwa ambaye ni mwamuzi mstaafu.

Uchaguzi uliahirishwa mara kadhaa kutokana na changamoto mbalimbali.

Wajumbe wengine wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni pamoja na Habyarimana Matiku ambaye amechaguliwa kuwa makamu wa rais, Kankindi Alida kama mkuu wa kitengo cha fedha, Rwenkunda Quita kama mkuu wa masoko na Mukangoboka Christine aliyechaguliwa kuwa mkuu wa soka la vijana.

Viongozi waliochaguliwa watahudumu kwa muda wa miaka minne.

Rais aliyekuwa akimaliza muda wake Vincent Nzamwita hakuwania nafasi hiyo kwa sababu binafsi.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana