Pata taarifa kuu
FIFA-CAS-PLATIN

Michel Platin awakashifu majaji waliomfungia kujihusisha na soka

Rais wa zamani wa shirikisho la mpira barani Ulaya UEFA Michel Platin amewataja majaji waliomuhukumu kutojihusisha na soka kwa muda wa miaka nane kuwa ni “ujinga” na kudai kuwa “atathibitisha ukweli”.

Michel Platini, mwezi Agosti 2014, katika mji wa Monte Carlo.
Michel Platini, mwezi Agosti 2014, katika mji wa Monte Carlo. REUTERS/Eric Gaillard/Files
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyu wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Juventus ya Italia alishuhudia adhabu yake ya kutojihusisha na soka kwa muda wa miaka 8 kutokana na kupkea malipo haramu ya dola milioni 2 za Marekani kutoka kwa rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter, ikipunguzwa kwa miaka miwili na majaji wa mahakama ya haki za binadamu mwezi Januari.

Lakini licha ya kuwa adhabu yake ilipunguzwa kwa miaka miwili na kuwa miaka minne kutokana na rufaa yake kwenye mahakama ya michezo CAS, Michel alidai kuwa hukumu aliyopewa kutojihusisha na soka hadi mwezi Octoba 2019 haikuwa ya haki.

“Siwezi kukubali kushindwa wakati nikiwa sijafanya kosa lolote. Wamenizuia nisifanye kazi kwenye mpira wa miguu kwa miaka minne! Hawa ni watu gani wa ajabu wanaonizuia?” alisema Platin.

“Majaji takataka wa FIFA na CAS hata sio majaji wa kweli.” aliongeza kiongozi huyo wa zamani kwenye soka.

Kuondolewa ofisini kwa Platin kulimfanya akose nafasi ya kumrithi Blatter kama raia wa FIFA, shirikisho ambalo sasa linaongozwa na aliyekuwa katibu wake mkuu UEFA, Gianni Infantino.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.