Pata taarifa kuu
CAF

CAF yatangaza hatua ya makundi taji la klabu bingwa na mtoano taji la shirikisho

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF limetoa ratiba ya hatua ya hatua ya makundi ya michuano ya ngazi ya klabu bingwa barani Afrika.

Ratiba ya makundi ya michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika, 2018.
Ratiba ya makundi ya michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika, 2018. Cafonline.com/twitter
Matangazo ya kibiashara

Katika ratiba hiyo kundi A litakuwa na timu za Al-Ahly ya Misri, Township Rollers ya Botswana, KCCA ya Uganda na Esperance ya Tunisia huku kundi B likiwa na timu za TP Mazembe ya DRC, MC Alger ya Algeria , Difaa El Jadida ya Morocco na ES Setif ya Algeria.

Kundi C lina timu za Mamelod Sundowns, AS Togo-Port ya Togo , bingwa mtetezi Wydad Casablanca ya Morocco na Horoya ya Guinea. Kundi D linajumuisha timu za Zesco United ya Zambia, Premiero Agosto ya Angola, Etoile Du Sahel ya Tunisia na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika zinatazamiwa kuanza kuchezwa mwezi wa sita.

Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika hatua nyingine CAF jana ilichezesha droo ya hatua ya mwisho ya taji la shirikisho barani huku Yanga ya Tanzania ikipangwa kuchuana na Waletya Dicha ya Ethiopia.

Yanga iliangukia kwenye michuano ya Shirikisho baada ya kuondolewa katika Ligi ya mabingwa Afrika na timu ya Township Rollers ya Botswana.

Ratiba ya mechi za kombe la Shirikisho barani Afrika, 2018.
Ratiba ya mechi za kombe la Shirikisho barani Afrika, 2018. Cafonline.com/twitter

Wawakilishi wengine wa Afrika Mashariki, klabu ya Gor Mahia ya Kenya itachuana na Supersports ya Afrika Kusini, huku Rayons Sports ya Rwanda ikitarajiwa kuchuana na Costal Du Sol ya Msumbiji.

Al Hilal ya Sudan itakabiliana na Akwa United ya Nigeria wakati ST. George ya Ethiopia itakabiliana na CARA Brazaville ya Congo.

Ratiba ya mechi nyingine za taji la shirikisho ni kama ifuatavyo:

Adouana Stars ya Ghana itacheza na Foisa Junior ya Madagascar, Williamsonville itacheza na Deportive Niefang, Plateau United itachuana na USM Alger.

Asec Mimosas itakuwa mwenyeji wa CR Belouizdad, Bidvest Wits itachuana na Enyimba, Generation Foot itachuana na RS Berkane, CF Mounana itakuwa mwenyeji wa Al-Masry, UD Songo itapambana na AL Hilal-AL Ubayyid wakati AS Vita club itacheza na CS la Mancha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.