Pata taarifa kuu
TANZANIA-CAF-SIMBA-YANGA

Simba, Yanga zashindwa kutamba michuano ya klabu bingwa na Shirikisho

Timu za Simba na Yanga za Tanzania zimeshindwa kutamba katika michuano ya ngazi ya klabu barani Afrika na kujikuta zikiondolewa mashindanoni.

-
- CAF
Matangazo ya kibiashara

Yanga ilitoka sare ya bila kufungana na Township Rollers ya Botswana na hivyo kutolewa mashindanoni kwa jumla ya mabao 2-1. Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliochezwa jijini Dar es Salaam ulimalizika kwa Yanga kuchapwa mabao 2-1.

Kwa matokeo hayo Yanga ambao ni mabingwa wa soka nchini Tanzania watashiriki hatua ya mtoano ya taji la shirikisho Afrika.

Simba iliyokuwa ugenini, ikihitaji ushindi dhidi ya Al Masry ilishindwa kutamba kwa sare ya bila mabao na hivyo kutolewa kwenye michuano ya shirikisho kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza baina ya timu hizo.

Mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es salaam, Simba na Al Masry zilifungana mabao 2-2.

Katika mchezo mwingine mabingwa wa mwaka 2015 wa taji la klabu bingwa Afrika TP Mazembe walifuzu hatua ya makundi licha ya kufungwa mabao 3-0 na timu ya Songo ya Msumbiji, mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ulimalizika kwa Mazembe kupata ushindi wa mabao 4-0.

Matokeo mengine ya Ligi ya Mabingwa

KCCA ya Uganda iliishinda ST. Georges ya Ethiopia kwa bao 1-0 na kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo.

Mbabane Swallows ya Swaziland iliishinda Zanaco ya Zambia kwa jumla ya mabao 2-0

Ratiba ya mechi za leo klabu bingwa

AS Vita ya DRC inaipokea Difaa Jadida ya Morocco

Esperance ya Tunisia inachuana na Gor Mahia ya kenya

ASEC Mimosas ya Ivory Coast itachuana na Zesco ya Zambia

Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini itapambana na Rayon Sports ya Rwanda

ES Setif ya Algeria itakabiliana na Adouana Stars ya Ghana.

Taji la Shirikisho

APR ya Rwanda ilitolewa mashindanoni na Djoliba licha ya kushinda mabao 2-1, ilifungwa kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.