Pata taarifa kuu
TFF-TANZANIA-WAMBURA

Makamu wa Rais wa TFF ahukumiwa kifungo cha maisha kujihusisha na soka

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF, imemuhukumu Makamu wa rais wa shirikisho hilo Michael Wambura baada ya kukutwa na makosa matatu.

Michael Wambura
Michael Wambura facebook
Matangazo ya kibiashara

Makosa yaliyokuwa yakimkabili kiongozi huyo ni Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

Makosa mengine ni Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013 na Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)

Kamati ya maadili iliyotoa uamuzi huo ilikutana jana Jijini Dar es Salaam na kupitia shauri hilo kabla ya kutoa uamuzi hii leo.

Katika uamuzi wake kamati ya maadili imeamuru Wambura alipe kiasi cha milioni 10 za Tanzania kwa kosa la kujihusisha na ufisadi

Kamati ya maadili pia imependekeza Michael Wambura afikishwe kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya uchunguzi huku pia ikipendekezwa viongozi wa zamani wa TFF, Jamal Malinzi aliyekuwa rais, Celestine Mwesigwa aliyekuwa katibu mkuu ambao walikuwepo wakati vitendo hivyo vikifanyika waunganishwe kwenye uchanguzi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.