Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Yanga FC yapoteza mchezo dhidi ya Rollers

media Wachezaji wa Yanga FC na Rollers FC ya Bostwana twitter.com

Yanga imeanza vibaya mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Township Rollers katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanawapa wakati mgumu Yanga kabla ya mchezo wa marudiano baina ya timu hizo utakaochezwa Mjini Gaberone nchini Botswana.

Mabao ya Rollers yalifungwa na Lempose Tshireletso dakika ya 11 kwa mkwaju mkali uliombabatiza kipa wa Yanga, Ramadhan kabwili huku bao la pili likifungwa na Motsholetsi Sokwe kipindi cha pili baada ya wachezaji wa timu hiyo kugongeana pasi zaidi ya 10 kabla ya mpira kumfikia mfungaji.

Bao la kufutia machozi la Yanga lilifungwa na mchezaji kutoka Zambia, Obrey Chirwa dakika ya 30 ya mchezo akimalizia pasi kiungo Papy Tshishimbi.

Matokeo ya michezo mingine ya Ligi ya mabingwa Afrika:-

Al Ahly ya Misri iliishinda FC Mounana ya Gabon kwa mabao 4-0.

FC Horoya ya Guinea iliichapa Generation ya Senegal mabao 2-1.

Etoile Sahel iliishinda Plateau mabao 4-2.

Ratiba ya michezo ya leo ni kama ifuatavyo:-

Gor Mahia ya Kenya inaipokea Esperance ya Tunisia.

Saint George ya Ethiopia inachuana na KCCA ya Uganda.

Zanaco ya Zambia inacheza na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Rayon Sports inachuana na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini.

Difaa Jadida ya Morocco inachuana na AS Vita Club ya DRC.

TP Mazembe inacheza na UD Songo ya Msumbiji.

Zesco ya Zambia inacheza na Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana