Pata taarifa kuu
BURUNDI-SOKA-NKURUNZIZA

Maafisa wa serikali ya Burundi washtakiwa baada ya rais Nkurunziza kujeruhiwa uwanjani

Maafisa wawili wa serikali ya Burundi wamezuiwa na kufunguliwa  mashtaka baada ya wachezaji wa mchezo wa soka kumjeruhi rais Pierre Nkurunziza uwanjani.

Rais Pierre Nkurunziza akiwa uwanjani katika siku za hivi karibuni
Rais Pierre Nkurunziza akiwa uwanjani katika siku za hivi karibuni AFP/PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni, timu ya mji wa Kiremba ilikuwa inamenyana na Allelua FC timu inayomilikiwa na rais Nkurunziza wakati tukio hilo lilipotokea.

Ripoti kutoka kwa Mawakili wa maafisa hao wa serikali zinasema maafisa hao wa serikali waliozuiwa ni Mkurugenzi wa mji wa huo Kiremba, Cyriaque Nkezabahizi na Naibu wake Michel Mutama ambao walikuwa wamewachukua wachezaji kumenyana na Allelua FC.

Wakimbizi kutoka DRC wanaoishi katika mji huo, ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa katika kikosi cha mji huo.

Inaelezwa kuwa wachezaji wa mji huo hawakufahamu kuwa walikuwa wanacheza na rais Nkurunziza na mara kwa mara,  walimshambulia kwa mpira na kumwangusha wakati wakimpokonya silaha.

Mara nyingi, rais huyo anapoichezea timu yake huwa anaachwa kufunga mabao rahisi bila ya wachezaji wa upinzani kumzuia kwa hofu kuwa wanacheza na mkuu wa nchi.

Nkurunziza mwenye umri wa miaka 54, mkufunzi wa zamani wa michezo katika Chuo Kikuu cha Burundi, anafahamika kama mpenda michezo na mbali na soka, anapenda kujishirikisha katika mchezo wa uogeleaji na kukimbiza baiskeli.

Amejenga uwanja wa soka wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 9,000 nyumbani kwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.