Pata taarifa kuu
CHAN 2018

Sudan yamaliza ya tatu michuano ya CHAN

Timu ya taifa ya soka ya Sudan imemaliza katika nafasi ya tatu katika michuano ya CHAN biana ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani, inayomalizika Jumapili, nchini Morocco.

Wachezaji wa Sudan wakisherehekea baada ya kupata medali ya shaba katika mashindano ya CHAN Februari 03 2018
Wachezaji wa Sudan wakisherehekea baada ya kupata medali ya shaba katika mashindano ya CHAN Februari 03 2018 http://www.cafonline.com/
Matangazo ya kibiashara

Sudan imeshinda medali ya shaba katika mashindano hayo baada ya kuishinda Libya mabao 4-2 baada ya kupigwa kwa mikwaju ya penalti.

Mchuano huo ulikwenda katika hatua hiyo baada ya sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida na ule wa ziada.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Sudan inayofunzwa na kocha kutoka Croatia Zdravko Logarusic na matokeo haya yamewashangaza wengi ambao hawakuipa nafasi ya kufanya vizuri katika mashindano haya.

Sudan ilianza mchuano huo kwa kupata bao la ufunguzi katika dakika ya nane ya mchuano huo kupitia mshambuliaji Walaaeldin Musa na kuonekana kutawala mchuano huo hadi dakika 84, wakati waliporuhusu Libya kusawazisha kupitia Salem Ablo, aliyefunga kwa kichwa.

Libya ilishinda taji la CHAN mwaka 2014, wakati michuano hii ilipoandaliwa nchini Afrika Kusini.

Mbali na mchuano huu, wenyeji Morocco watamenyana na Nigeria katika fainali ya mchuano huu utakaopigwa katika uwanja wa Mohammed V mjini Casablanca.

Mshindi katika fainali hii atajishindia taji na Dola za Marekani Milioni 1.25.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.