Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 13/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Tanzania: Klabu ya Simba yamfuta kazi kocha Joseph Omog

media Joseph Omog kocha wa zamani wa klabu ya soka nchini Tanzania Simba, katika mojawapo ya mechi za ligi kuu nchini humo mwaka 2017 Goal.com

Klabu ya Simba SC ya Tanzania imemfukuza kazi kocha wake Joseph Omog siku moja baada ya Simba kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kufungwa na Green Worriers.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo jioni hii imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano ya pande mbili, baina ya uongozi na Joseph Omog.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kocha msaidizi, Mrundi Masoud Djuma ataendelea kusimamia timu wakati ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda ya Mtwara utakaochezwa mwishoni mwa wiki ijayo.

Kabla ya uamuzi huo mashabiki na wadau mbalimbali wa Simba akiwemo mwanahisa Mkuu Mohammed Dewji leo wametumia mitandao ya kijamii kupaza sauti ya kumtaka Omog ajiuzulu.

Omog alijiunga na Simba mwaka 2016 akitokea nyumbani kwao nchini Cameroon na amewahi kuifundisha Azam ya tanzania na AC Leopard ya Jamhuri ya Kongo ambayo mwaka 2012 aliiwezesha kushinda taji la shirikisho barani Afrika.

Ripoti ya mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana