Pata taarifa kuu
SOKA-CECAFA

Uganda kuanza kutetea taji la CECAFA

Timu ya soka ya Uganda itaanza kampeni ya kutetea taji la Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA dhidi ya Burundi.

Mashabiki wa Uganda Cranes
Mashabiki wa Uganda Cranes ©Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Huu ni mchuano wa tatu tangu kuanza kwa michuano hii mwishoni mwa wili iliyopita nchini Kenya.

Mchuano huu utachezwa Jumatatu jioni katika uwanja wa Bukhungu mjini Kakamega.

Kocha wa Uganda Cranes Moses Basena, amekiteua kikosi kilicho na wachezaji wengi chipukizi ikilinganishwa na wapinzani wao ambao wana kikosi chenye wachezaji wazoefu.

Wenyeji Kenya walianza vema kwa kuwashinda Rwanda mabao 2-0.

Mabao ya Harambee Stars yalifungwa na Mosoud Juma na Duncan Otieno katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Wageni walioalikwa katika michuano hii Libya, nao walianza kwa sare ya 0-0 dhidi ya Tanzania bara.

Kenya inaongoza kundi la A, kwa alama 3 huku Libya na Tanzania zikiwa na alama moja.

Ratiba Jumanne Desemba 5 2017:-

Zanzibar vs Rwanda

Kenya vs Libya

Sudan Kusini vs Ethiopia

Desemba 7 2017

Tanzania vs Zanzibar

Rwanda vs Libya

Burundi vs Ethiopia

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.