Pata taarifa kuu
CAF-CHAN-MISRI

CAF yasema Misri haijawapa taarifa ya kutoshiriki michuano ya CHAN

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linasema halijapokea barua rasmi kutoka kwa Shirikisho la soka nchini Misri, kuonesha nia yao ya kutoshiriki katika michuano ya CHAN mwaka ujao nchini Morocco.

Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF
Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF http://www.cafonline.com/
Matangazo ya kibiashara

Mapema wiki hii, viongozi wa soka nchini Misri walisema kuwa, timu ya taifa inayowajumuisha wachezaji wa ndani isingeweza kushiriki katika michuano hiyo kwa sababu, ya ratiba ngumu ya ligi kuu nchini humo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la soka Tharwat Sweilam amesema tayari wameiambia CAF kuwa hawatakuwepo katika michuano hiyo.

Mapema mwezi huu, uongozi wa soka barani Afrika, uliamua kuipa nafasi Misri kushiriki katika michuano hii baada ya kuipokonya Kenya haki za kuandaa michuano hiyo.

Misri haijawahi kushiriki katika michuano hii iliyoanza mwaka 2009 nchini Ivory Coast.

Misri ni mioongoni mwa mataifa 16, yaliyopangwa kushiriki katika makala ya tano ya michuano hiyo katika miji ya Agadir, Casablanca, Marrakech na Tangier kati ya tarehe 12 mwezi Januari na Februari 4 mwaka 2018.

Mataifa yatakayoshiriki ni pamoja na Morocco, Misri, Libya, Guinea, Mauritania, Nigeria, Ivory Coast, Burkina Faso, Equitorial Guinea, Congo, Cameroon, Uganda, Sudan, Angola, Namibia na Zambia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.