Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Ronaldo mchezaji bora wa dunia wa Fifa, Messi, Neymar waambulia patupu

media Mchezaji wa Real Madrid Christian Ronaldo akibusu tuzo aliyoshinda baada ya kukabidhiwa jijini London. 23 Octoba 2017 Images via Reuters/John Sibley

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid Christian Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia inayotolewa na shirikisho la soka la dunianik Fifa kwa mwaka 2017 katika sherehe zilizofanyika jijini London, Uingereza.

Mchambuliaji huyu wa Real Madrid ameshinda mpinzani wake wa karibu Lionel Messi wa FC Barcelona na mshambuliaji wa PSG yha Ufaransa Mbrazil Neymar.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 32, aliisadia klabu yake kutwaa taji la klabu bingwa barani Ulaya pamoja na kombe la ligi msimu wa mwaka 2016-2017.

Kwa upande wa wanawake mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya Barcelona Lieke Martens alishinda tuzo hiyo, huku kwa upande wa kocha bora wa mwaka, kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane alishinda tuzo hiyo huku kocha wa wanawake wa timu ya taifa ya Uholanzi Sarina Wiegman akichukua tuzo hiyo.

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Olivier Giroud alipokea zawadi ya goli bora la mwaka 2017 maarufu kama Puskas, baada ya kuifungia timu yake kwa mtindo ya Scorpion (Nge) wakati timu yake ikicheza na Crystal Palace mwezi Januari.

Hizi ni tuzo za pili za mchezaji bora wa dunia zinazotolewa na Fifa ambazo ni tofauti na ile tuzo ya Ballon d’Or.

Tuzo za Ballon d’Or zimekuwa zikitolewa na jarida la Ufaransa linaloandika masuala ya soka tanguj mwaka 1956, lakinik shirikisho la soka Fifa liliamua kumaliza ushirikiano wa utoaji wa tuzo hizi.

Badala yake Fifa ilizindua tuzo zake za dunia na Ronald ndiye alikuwa mchezaji wa kwanza kushinda msimu uliopita mwezi Januari.

Kura za kuchagua mchezaji bora na kocha bora zilipigwa na manahodha wa timu za taifa na makicha wao, waandishi wa habari walioteuliwa na kwa mara ya kwanza mashabiki wa soka walipiga kura kupitia kwenye mtandao kwa asilimia 25.

Katika kikosi cha dunia cha Fifa, kumefanyika mabadiliko kadhaa ukilinganisha na kile kikosi cha mwaka 2016 ambapo mlinda mlango wa Juventus Gianluigi Buffon amechukua nafasi ya kipa Manuel Neuer wa Bayern Munich, wakati beki wa AC Milani Leonardo Bonucci akichukua nafasi ya Gerard Pique wa Barcelona huku mshambuliaji Neymar akichukua nafasi ya Luis Suarez kwenye nafasi ya ushambuliaji.

Kikosi bora cha mwaka kinajumuisha wachezaji watano kutoka Real Madrid, wawili kutoka Barcelona, wawilik kutoka PSG na mmoja kutoka Juventus na mmoja kutoka AC Milan. Hakuna mchezaji yeyote kutoka ligi kuu ya Uingereza aliyejumuishwa kwenye kikosi hicho.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana