Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO

Argentina, Uruguay na Paraguay kuandaa kombe la dunia mwaka 2030

Nchi tatau kutoka bara la Amerika ikiwa ni pamoja na Argentina, Uruguay na Paraguay wamewasilisha maombi ya pamoja kuanda kombe la dunia mwaka 2030.

Mkutano wa kwanza wa kuanda ombi la pamoja la kuandaa kombe la dunia mwaka 2030 utafanyika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.
Mkutano wa kwanza wa kuanda ombi la pamoja la kuandaa kombe la dunia mwaka 2030 utafanyika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Kombe la dunia la mwaka 2030 litakuwa maadhimisho ya karne moja tangu mashindano hayo yaanze mwaka 1930.

Marais wa nchi hizi tatu walitangaza mpango huo mjini Buenos Aires siku ya Jumatano Oktoba 4. Hata hivyo zoezi la kumtafua mwandalizi litaanza miaka kadhaa ijayo.

Mkutano wa kwanza wa kuanda ombi hilo la pamoja utafanyika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.

Uruguay imetoa ombi lake hilo wakati inasherehekea miaka 100 kama nchi ya kwanza kabisa kuandaa kombe la dunia.

Wakati huo huo Marekani, Mexico na Canada walitoa ombi la kuanda kombe la dunia mwaka 2026.

Katika kombe la mwaka 2026, jumla ya timu 48, badala ya 32 zitashindana. Hayo ni kufuatia mabadiliko yaliyotangazwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) mapema mweka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.