Pata taarifa kuu
SOKA-PSG-MAYERN MUNICH-MICHEZO

PSG waibwaga Bayern katika Ligi ya Mabingwa

Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) imeicharaza Bayern Munich wa mabao 3-0 katika kundi B katika michuano ya Ligi ya Mabingwa (UEFA) Septemba 27, 2017.

Neymar, Dani Alves, Kylian Mbappé, Edinson Cavani na Marquinhos (kutoka kushoto kwenda kulia) wakisherehekea bao la kwanza la PSG dhidi ya Bayern Munich.
Neymar, Dani Alves, Kylian Mbappé, Edinson Cavani na Marquinhos (kutoka kushoto kwenda kulia) wakisherehekea bao la kwanza la PSG dhidi ya Bayern Munich. RFI / Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Paris Saint-Germain (PSG) wanaendelea vizuri katika msimu huu, wakiwa na ushindi tisa katika mechi kumi walizocheza.

Baada ya kuibwagiza Glasgow mabao 5-0, PSG wameipa soma kubwa Bayern Munich katika michuano ya Kombe la Ulaya (Ligi ya Mabingwa UEFA).

Baada ya sekunde 85, kungo wa kulia Dani Alves amepachika bao la kwanza kwa kupitisha mpira kati ya miguu ya kipa Sven Ulreich.

Bao la pili liliwekwa kimyani na Cavani, huku bao la tatu likiingizwa na Neymar katika dakika ya 63 ya mchezo.

Michuano ya Ligi ya Mabingwa (UEFA) inatarajiwa kuchezwa hii Leo kwa michezo kadhaa ikiwa ni hatua ya makundi.

FC Astana ni wenyeji wa Slavia Prague, Partizan Beograd wanawaalika Dynamo Kyiv, Skenderbeu ni wenyeji wa Young Boys, FC Cologne watamenyana na FK Crvena Zvezda, AC Milan ni wenyeji wa Rijeka.

Bate Borisov wanacheza na Arsenal, Salzburg dhidi ya Marseille, Zenit wanawakaribisha Sociedad, Everton ni wenyeji wa Apollon, Locomotiv watakuwa ni wenyeji wa Fastav, Maccabi Tella Viv wanawaalika Vilareal , Lyon inamenyana na Atalanta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.