Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SENEGAL-SOKA

Mchezo kati ya Afrika Kusini na Senegal kurudiwa

Shirikisho la Kimataifa Soka FIFA, limetangaza kwamba mchezo kati ya Afrika Kusini na Senegal unapaswa kurudiwa kutokana na makosa ya mwamuzi wa mchezo huo.

Bafana bafana, timu ya taifa ya soka ya Afrika Kusini.
Bafana bafana, timu ya taifa ya soka ya Afrika Kusini. AFP/Alexander Joe
Matangazo ya kibiashara

Mchezo Kati ya Bafana BAfana na Senegal ulipigwa Novemba 12, ambapo hadi timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana waliibuka mshindi.

Kwa mujibu wa maafisa wa FIFA, mchezo huo utarudiwa Novemba 2017 katika kalenda ya kimataifa.

Hata hivyo haijatajwa tarehe ambayo itazikutanisha tena timu hizi mbili.

FIFA imetoa uamuzi huo baada ya mwamuzi wa mchezo Joseph Lamptey kuharibu huo. FIFA imesema Bw Lamptey ameadhibiwa na Kamati yake ya nidhamu ya FIFA.

Mwamuzi Joseph Lamptey raia wa Ghana amefungiwa kutojihusisha na masuala ya soka maisha yake yote baada ya kukutwa na hatia ya kupanga matokeo.

Mwamuzi huyu aliizawadia Afrika Kusini adhabu ya penati katika mchezo uliyopata na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Senegal mwezi Novemba mwaka jana kwa kile muamuzi alidai ni mchezaji wa Senegal Kalidou Koulibaly aliushika mpira kwenye eneo la hatari wakati ulimgonga kwenye goti.

Lamptey alikuwa amefungiwa maisha mwezi Machi mwaka huu lakini Jumatano ya wiki hii mahakama ya kimataifa ya michezo CAS iliunga mkono adhabu hiyo.

Kwenye msimamo wa sasa kwenye kundi lao timu ya Senegal na Afrika Kusini zinashikilia nafasi ya tatu na ya nne kwenye kundi D nyuma ya Burkina Faso na Cape Verde.

Ni timu ambazo zitakuwa kileleni katika kila kundi ndizo zitakazofuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwakani nchini Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.