Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA-SOKA

Cameroon yashindwa kufuzu fainali ya kombe la dunia

Cameroon haiwezi kufuzu katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Nigeria jijini Yaounde Jumatatu usiku.

Kocha wa  timu ya taifa ya Cameroon  Hugo Broos
Kocha wa timu ya taifa ya Cameroon Hugo Broos Reuters / Amr Abdallah Dalsh Livepic
Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo yana maanisha kuwa Cameroon wana alama tatu kati ya mechi nne ilizocheza na hivyo haiwezi kuongoza kundi lao na kufuzu katika fainali hiyo.

Kuelekea mchuano huu kocha wa Cameroon Hugo Broos alisema kuwa ingekuwa vigumu sana kwa vijana wake kufuzu katika fainali hiyo kwa sababu walihitaji kushinda mechi tatu zinazosalia, jambo ambalo halingewezekana.

Cameroon imewahi kufuzu katika fainali hii mara saba mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2014 nchini Brazil.

Mbali na mchuano huo, Libya nao walipata ushindi wao wa kwanza katika kundi A baada ya kuishinda Guinea bao 1-0.

Ikiwa Tunisia itapata alama yoyote dhidi ya DR Congo siku ya Jumanne, basi Libya na Guinea watakuwa wameondolewa katika michuano hiyo.

Uganda Cranes walioishinda Misri mabao 2-1 wiki iliyopita, leo wana kibarua kutafuta alama tatu muhimu kama ilivyokuwa jijini Kampala.

Ratiba kamili ya mechi za Jumanne, Septemba 5 2017:-

  • Congo v Ghana
  • Afrika Kusini v Cape Verde
  • DR Congo v Tunisia
  • Cote d'Ivoire v Gabon
  • Burkina Faso v Senegal
  • Misri v Uganda
  • Mali v Morocco
  • Algeria v Zambia

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.