Pata taarifa kuu
TENNIS-US OPEN

Federer na Nadal waanza vema mashindano ya US Open

Roger Federer bingwa mara tano wa mashindano ya Tennis ya US Open, alianza vema mashindano ya mwaka huu baada ya kumshinda Mmarekani Frances Tiafoe katika mzunguko wa kwanza.

Roger Federer akisherehekea baada ya kupata ushindi
Roger Federer akisherehekea baada ya kupata ushindi Andrew Couldridge/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Federer raia wa Uswizi mwenye umri wa miaka 36, alihitajika kucheza seti tano kushinda mchuano huo.

Baada ya mchuano huo, Federer alishinda kwa kupata 4-6,  6-2,  6-1, 1-6,  6-4 katika uwanja wa Arthur Ashe.

Mbali na Federer, bingwa nambari moja duniani Mhispania Rafael Nadal, alimshinda Mserbia Dusan Lajovic kwa seti za 7-6,  (8-6),  6-2,  6-2.

Matokeo ya wanawake:-

Karolina Pliskova (Jamhuri ya Czech) alimshinda Magda Linette (Kutoka Poland) kwa seti za 6-2, 6-1

Barbora Strycova (Jamhuri ya Czech) alimshinda Misaki Doi (kutoka Japan) kwa seti za 6-1, 6-3.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.