Pata taarifa kuu
MASUMBWI

Floyd Mayweather na Conor McGregor kupambana katika pigano la kihistoria

Wanamasumbwi Floyd Mayweather kutoka Marekani na Conor McGregor kutoka Ireland, watapambana katika pigano linaloelezwa kuwa la kitajiri zaidi kihistoria, kuwania ubingwa wa WBC, katika ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Nevada nchini Marekani.

Wanamasumbwi Floyd Mayweather kutoka Marekani na Conor McGregor kutoka Ireland wakiangalia usoni baada ya pambano lao kutangazwa
Wanamasumbwi Floyd Mayweather kutoka Marekani na Conor McGregor kutoka Ireland wakiangalia usoni baada ya pambano lao kutangazwa PHOTO | ETHAN MILLER | AFP
Matangazo ya kibiashara

Litakuwa ni pigano la raundi 12, litakalooneshwa kupitia runinga katika mataifa 200 kote duniani.

Waandalizi wa pigano hili wanasema wanatarajiwa kupata Dola Milioni 600 na kupita kiasi kilichopatikana wakati wa pigano dhidi ya Manny Pacquiao, na Mayweather.

Mayweather anatarajiwa kulipwa Dola Milioni 100 baada ya pigano hilo huku McGregor akipata Dola Milioni 75 kwa mujibu wa mkataba waliotia saini mwezi Juni.

Kuelekea katika pigano hili McGregor mwenye umri wa miaka 29, amesema analenga kumshinda Mayweather ndani ya raundi mbili za kwanza.

Katika mapigano 24 aliyopigana, ameshinda 21 na 18 kupitia knockout na kushindwa mapigano matatu.

Floyd Mayweather mwenye umri wa 40, naye anakwenda katika pigano hili akiwa hajapoteza mchuano wowote katika mapigano 49 aliyopigana.

Mapigano 26, ameshinda kwa knockout.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.