Pata taarifa kuu
SOKA-UGANDA

Geofrey Sserunkuma mchezaji bora nchini Uganda

Mshambuliaji wa klabu ya KCCA nchini Uganda Geofrey Sserunkuma, ndio mchezaji bora wa msimu wa soka msimu uliopita nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Sserunkuma aliyepewa zawadi ya gari kuonesha  juhudi zake, aliibuka pia mshindi wa taji hilo kwa kufunga mabao mengi na kuisaidia klabu yake kushinda ligi kuu ya soka msimu uliopita.

Sherehe za tuzo hiyo zilifanyika jijini Kampala na kuhudhuriwa na rais wa Shirikisho la soka nchini humo Moses Magongo na wadau wengine wa soka nchini humo.

Aidha, tuzo hizi zimekuja wakati huu msimu unapotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Klabu ya KCCA itaiwakilisha Uganda katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika CAF, mwaka ujao.

Tuzo

  • Mchezaji bira na mwenye thamani kubwa: Geofrey Sserunkuma (KCCA )
  • Mfungaji bora: Geofrey Sserunkuma (KCCA ) alifunga mabao 21
  • Mchezaji aliyependwa na mashabiki: Geoffrey Sserunkuma (KCCA )
  • Mchezaji chipikuzi wa mwaka-Allan Okello (KCCA FC)
  • Kiungo wa Kati wa mwaka: Saddam Juma (Express)
  • Kipa bora wa mwaka: Ismail Watenga (Vipers)
  • Beki bora wa mwaka: Halid Lwaliwa (Vipers)
  • Kocha bora wa mwaka kwa makipa: Stephen Billy Kiggundu (Vipers)
  • Kocha bora wa mwaka: Mike Mutebi (KCCA FC)
  • Refarii bora wa mwaka: Alex Munabi

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.