Pata taarifa kuu
CAF-SOKA

Mkutano Mkuu wa CAF kuamua mfumo mpya wa fainali za AFCON

Fainali ya mchezo wa soka kuwania ubingwa wa Afrika AFCON, huenda ikaanza kuchezwa mwezi Juni au Julai ikiwa mapendekezo haya yataidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF.

New Caf President Ahmad Ahmad
New Caf President Ahmad Ahmad Goal.com
Matangazo ya kibiashara

Mapendekezo haya yamekuja baada ya kubainika kuwa wakati wa fainali hiyo mwezi Januari na Februari, wachezaji wengi wa Afrika huwa wanashindwa kujigawa au hata kuja kuchezea timu zao za taifa kwa sababu michuano ya ligi kuu barani Ulaya wanakocheza huwa zimeshika kasi.

Aidha, imependekezwa kuwa mataifa yanayoshiriki katika fainali hiyo iongezwe na kufikia nchi 24 kutoka 16.

Uamuzi wa mwisho utaamuliwa na wajumbe wanaokutana mjini Rabat  nchini Morocco siku ya Ijumaa, watakapopigia kura mapendekezo haya.

Wachezaji wa zamani lakini pia makocha maarufu barani Afrika wanashiriki katika mkutano huu ili kutoa mapendekezo yao.

Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF Ahmad Ahmad amesema kuwa anaamini kuwa mabadiliko haya ni muhimu na yatasaidia kuimarisha soka barani Afrika.

Mbali na michuano baina ya timu za Afrika, huenda ratiba ya michuano ya klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika ikabadilishwa.

Fainali ya michuano hii huchezwa mwezi Novemba kila mwaka. Mabadiliko haya yaliahidiwa na Ahmad wakati akitafuta urais wa CAF mapema mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.