Pata taarifa kuu
RIADHA-IAAF-KENYA

Kenya yafanikiwa pakubwa kuandaa mashindano ya riadha ya dunia baina ya vijana

Kenya imejiweka katika nafasi nzuri duniani baada ya kufanikiwa kuandaa mashindano ya riadha ya dunia kwa vijana wasiozidi miaka 18 iliyokamilika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Nairobi.

Mwanariadha wa Kenya Jackline Wambui alivyoshinda  mbio za Mita 800.
Mwanariadha wa Kenya Jackline Wambui alivyoshinda mbio za Mita 800. www.iaaf.org
Matangazo ya kibiashara

Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani ulikuwa mwenyeji wa wanariadha zaidi ya wanariadha 1400 wakishiriki kutoka Mataifa 130.

Yalikuwa ni makala ya 10 na ya mwisho ya mashindano haya yanayoandaliwa na Chama cha riadha duniani IAAF, ambacho kimesema mashindano haya ya kila baada ya miaka miwili, sasa yatakuwa yanaandaliwa katika mabara mbalimbali.

Makala ya kwanza ya mashindano haya yalifanyika mwaka 1999 jijini Bydgoszcz nchini Poland .

Afrika Kusini ilimaliza ya kwanza kwa medali 11, tano za dhahabu, tatu za fedha na zingine tatu za shaba.

Wanariadha hao walifanya vizuri katika mbio fupi za Mita 100, 200 na 400 kupokezana kijiti kwa wavulana huku wanawake pia wakifanya vizuri pia katika mbio za Mita 400 kupokezana vijiti kwa upande wa wanawake.

China iliibuka ya pili pia kwa medali 11 huku Cuba ikiwa ya tatu kwa medali nane, tano za dhahabu, mbili za fedha na moja ya shaba.

Sikiliza uchambuzi.

Wenyeji Kenya ndio waliojipatia medali nyingi zaidi katika mashindano haya kwa kupata medali 15. Nne za dhahabu, saba za fedha na nne za shaba.

Wanariadha wa Kenya walinawiri katika mbio za Mita 1500 kwa wavulana huku George Meitamei Manangoi akishinda dhahabu, huku Leonard Kipkemoi Bett akishinda medali katika mbio za Mita 2000 kuruka viunzi na maji kwa wavulana na wasicha.

Jackline Wambui akishinda mbio za Mita 800.

Ethiopia ilimaliza ya tano kwa medali 12, zikiwemo nne za dhahabu ambazo Melese Mberet alishinda mbio za Mita 800 kwa wanaume, Selemon Barega kwa wavuluana mbio za Mita 3000 huku Lemlem Hailu akishinda mbio za Mita 1500.

Abersh Minsewo alishinda mbio za Mita 3000 kwa upande wa wanawake.

Maelfu ya wapenzi wa ridhaa walifurika kujionea mashindano hayo makubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.