Pata taarifa kuu
SOKA-KOMBE LA MABARA

Cameroon kutafuta ushindi muhimu dhidi ya Australia

Timu ya taifa ya soka ya Cameroon inashuka dimbani katika mchuano wake wa pili kupambana na Australia kuwania kombe la dunia baina ya mabara inayoendelea nchini Urusi.

Timu ya taifa ya Cameroon ilivyomenyana na Chile katika mchuano wake wa ufunguzi kuwania taji la dunia la mabara nchini Urusi
Timu ya taifa ya Cameroon ilivyomenyana na Chile katika mchuano wake wa ufunguzi kuwania taji la dunia la mabara nchini Urusi wordpress.com
Matangazo ya kibiashara

Kocha Hugo Broos amesema anaamini mchuano wa leo utawapa ushindi baada ya kupoteza mchuano wa ufunguzi wa kundi B dhidi ya Chile kwa mabao 2-0.

Aidha, amewataka wachezaji wake kuwa makini uwanjani na kuwoanya kutoidharau Australia na kuiona kama timu rahisi.

Ameongeza kuwa lengo lao ni kupata ushindi na kutawala katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Mchuano huu ni muhimu sana kwa wawakilishi hawa wa bara Afrika kwa sababu wanahitaji ushindi ili kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Ujerumani ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la dunia, watamenyana na Chile katika mchuano wake wa pili.

Walianza vema mchuano wake wa kwanza baada ya kuishinda Australia mabao 3-2.

Siku ya Jumatano, Ureno waliifunga wenyeji Urusi bao 1-0 huku Mexico wakiwashinda New Zealand mabao 2-1.

Mexico na Ureno inaongoza kundi hilo kwa alama nne.

Mechi za mwisho za kundi hili zitachezwa sku ya Jumamosi, Mexico dhidi ya Urusi na New Zealand ambao hawana nafasi ya kusonga mbele dhidi ya Ureno.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.