Pata taarifa kuu
SOKA-CAF-KLABU BINGWA-SHIRIKISHO

Matumaini ya AS Vita Club kusonga mbele yaanza kudidimia

Matumaini ya klabu ya soka ya AS Vita Club kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuzu katika hatua ya robo fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika CAF, yameanza kudidimia baada ya kupoteza mechi yake ya tatu katika hatua ya makundi.

Klabu ya Saint George ya Ethiopia baada ya kuishinda AS Vita Club ya DRC
Klabu ya Saint George ya Ethiopia baada ya kuishinda AS Vita Club ya DRC Cafonline
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa wiki iliyopita, AS Vita Club ilifungwa na Saint George ya Ethiopia bao 1-0, mechi iliyochezwa katika uwanja wa taifa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Bao hilo la pekee la ushindi lilikuja katika dakika 59, kipindi cha pili baada ya Saladin Said kutikisa nyavu ya AS Vita Club.

Matokeo haya yanamaanisha kuwa AS Vita Club ni ya mwisho katka kundi C bila ya alama yoyote, nyuma ya mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns ambao ni wa tatu kwa alama nne.

Kundi hili linaongozwa na Esperance de Tunis ya Tunisia kwa alama 7 baada ya kushinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza.

AS Vita Club inasalia na mechi tatu kumaliza kundi hili, dhidi ya Saint George tarehe 20 mwezi Juni jijini Kinshasa lakini pia itakuwa ugenini kumenyana na Esperance de Tunis na kumalizia Mamelodi Sundowns.

Nao mabingwa watetezi wa michuano ya Shirikisho, TP Mazembe wana kibarua kigumu cha kutetea taji hilo kutokana na namna mambo yalivyo katika kundi la D.

Sare ya mabao 2-2 dhidi ya Supersport United, hayakuwa matokeo mazuri kwa mabingwa hao waliokuwa nyumbani katika uwanja wao wa Kamalondo mjini Lubumbashi.

Wachezaji wa klabu ya Supersport United katika maandalizi kabla ya kumenyana na TP Mazembe na kutoka sare ya mabao 2-2
Wachezaji wa klabu ya Supersport United katika maandalizi kabla ya kumenyana na TP Mazembe na kutoka sare ya mabao 2-2 cafonline

Mazembe waliaza vema sana kwa kupata mabao mawili katika dakika ya 21 na 25 kupitia Ben Malango na Rainford Kalaba lakini dakika moja baadaye, Aubrey Modiba aliifungia klabu yake na baadaye Teboho Mokoena akaisawazishia klabu yake katika dakika 65 ya mchuano huo.

KCCA ya Uganda nayo imekuwa na matokeo mazuri baada ya ksuhinda mechi yake ya pili katika kundi A.

Wakicheza nyumbani katika uwanja wa Philip Onyango jijini Kampala, waliishinda Rivers United mabao 2-1.

Derrick Nsibambi ndiye aliyekuwa shujaa wa mechi hiyo baada ya kuifungia KCCA mabao yote mawili.

Matokeo haya yameifanya KCCA NA FUS Rabat kuwa na alama 6, mbele ya Club Africain na Rivers United.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.