Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

TP Mazembe yaanza kwa ushindi huku Mamelodi Sundowns ikibanwa na Saint George

media Wachezaji wa MC Ager na Platinum Stars wakimenyana mwishoni mwa juma lililopita Cafonline

Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo ndio mabingwa watetezi wa taji la klabu bingwa barani Afrika ilianza kwa sare ya kutofungana katika mchuano wake wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Saint George ya Ethiopia mwishoni mwa juma lililopita.

Hata hivyo, Esperance de Tunis ya Tunisia ikicheza nyumbani mjini Rades, ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya AS Vita Club ya DRC.

Kundi hili linaongozwa na Esperance de Tunis kwa alama 3, ikifuatwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa alama moja.

Mechi ya mzunguko wa pili zitapigwa tarehe 23 mwezi huu wa Mei.

Saint George itakuwa nyumbani kumenyana na Esperance de Tunis, huku AS Vita Club ikipambana na Mamelodi Sundowns.

Matokeo mengine:

Kundi A
Etoile du Sahel 5-0 Ferroviario Beira
Al Hilal 1-1 Al-Merrikh

Kundi B
USM Alger 3-0 Al-Ahli Tripoli
Zamalek 2-CAPS United

Kundi D
Wydad Casablanca 2-0 Coton Sport
Al-Ahly 0-0 Zanaco

Katika michuano ya Shirikisho, klabu ya KCCA ya Uganda ilianza vibaya ugenini baada ya kufungwa na FUS Rabat ya Morocco mabao 3-0.

Club Africain ya Tunisia nayo ilianza vema kwa kushinda Rivers United ya Nigeria mabao 3-1.

Mabingwa watetezi TP Mazembe ya DRC ambao wapo katika kundi D, walianza vema baada ya kuishinda CF Mounana ya Gabon kwa mabao 2-0, huku SuperSport United ya Afrika Kusini ikitoka sare ya mabao 2-2 na Horoya ya Guinea.

Matokeo mengine:

Kundi la C

ZESCO United 1-0 Smouha
Recreativo do Libolo 1-0 Al Hilal Al-Ubayyid

Kundi B:
CS Sfaxien 1-0 Mbabane Swallows
Platinum Stars 1-1 MC Alger
 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana