Pata taarifa kuu
SOKA-UEFA

Real Madrid kumenyana na Juventus katika fainali ya UEFA msimu huu

Mabingwa mara 11 wa taji la klabu bingwa barani Ulaya UEFA, Real Madrid ya Uhispania, itamenyana na mabingwa mara mbili Juventus ya Italia kuwania taji la msimu huu.

Wachezaji wa Real Madrid Isco na Benzema, baada ya kufuzu katika hatua ya fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya
Wachezaji wa Real Madrid Isco na Benzema, baada ya kufuzu katika hatua ya fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya euters / Juan Medina
Matangazo ya kibiashara

Mechi ya fainali itachezwa tarehe 3 mwezi Juni katika uwanja wa Millennium mjini Cardiff nchini Uingereza.

Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa taji hili, walifuzu katika hatua ya fainali kwa mara nyingine baada ya ushindi wa jumla ya mbao 4-2 dhidi ya Atletico Madrid pia ya Uhispania baada ya mechi za nyumbani na ugenini.

Juventus nayo ilifuzu baada ya kuilemea Monaco ya Uhispania kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya kushinda nyumbani na ugenini mecho zote mbili za nusu fainali.

Timu hizi mbili zimekutana hapo awali katika michuano hii mara 18.

Kipindi hicho chote, timu zote mbili zimeshinda mechi 8 na kutoka sare mara mbili.

Mara ya mwisho kwa timu hizi mbili kukutana katika fainali ya taji hili mwaka 1997, fainali ambayo Madrid walishinda bao 1-0 na kushinda taji lake la saba.

Real Madrid ambayo imefika katika hatua ya fainali mara 15 imeshinda taji hili mwaka 1955–56, 1956–57, 1957–58, 1958–59, 1959–60, 1965–66, 1997–98, 1999–2000, 2001–02, 2013–14, 2015–16.

Juventus nayo imewahi kucheza katika fainali sita, imeshinda mwaka 1984–85, 1995–96.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.