Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Mechi ya AFC Leopards na Gor Mahia kuchezwa uwanjani Nyayo siku ya Jumapili

media Tangazo la mchuano kati ya Gor Mahia na AFC Leopards superfoota.co.ke

Mchuano wa soka wa ligi kuu nchini Kenya kati ya watani wa jadi Gor Mahia na AFC Leopards, utachezwa siku ya Jumapili licha ya hapo awali kuahirishwa kwa sababu za kiusalama.

Kampuni ya KPL inayosimamia ligi kuu ya soka nchini humo imeeleza kuwa AFC Leopards imefanikiwa kuupata uwanja wa taifa wa Nyayo kuandaa mchuano huo maarufu kama Nairobi Derby au Mashemaji Derby.

Mchuano huu awali ulikuwa umepangwa kufanyika katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru, lakini uongozi wa soka ukaamua kuahirisha kwa sababu za kiusalama kutokana na wingi wa mashabiki wa timu hizo mbili.

Kanuni za ligi kuu ya soka nchini humo, zinaitaka klabu mweyeji kuhakikisha kuwa inashughulikia maswala ya usalama na mambo mengine.

Viwanja viwili vikubwa nchini humo Kasarani na Nyayo vilivyo jijini Nairobi, vimefungwa kwa maandalizi ya michuano ya mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN.

AFC na Gor Mahia vitamenyana kwa mara ya 83 katika historia ya ligi kuu ya soka nchini humo.

Uongozi wa klabu ya AFC umetoa wito kwa mashabiki wake kujitokeza kwa wingi, kuishabiki klabu yao maarufu kama Ingwe.

Gor Mahia ambao ni mabingwa wa mwaka 2015, ni wa pili latika msururu wa ligi hiyo kwa alama 16 baada ya mechi nane, huku AFC Leopards ikiwa ya nne kwa alama 14 baada ya mechi nane pia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana