Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Kombe la Dunia 2018: Japani waibwagiza Colombia 2-1 na kuchukua nafasi ya kwanza katika kundi H
Michezo

Kenya yafuzu robo fainali ya michuano ya dunia ya HSBC nchini Singapore

media Wachezaji wa Kenya katika mchuano wao dhidi ya Argentina siku ya Jumamosi Aprili 15 2017 HSBC World Rugby Sevens

Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya wachezaji saba kila upande ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Singapore HSBC World Rugby Sevens , imefuzu katika hatua ya robo fainali.

Hii ina maana kuwa Kenya ipo katika nafasi nzuri ya kutetea taji lake, ililoshinda mwaka uliopita.

Kenya ilifuzu katika hatua hii baada ya kuishinda Samoa kwa alama 17-7  na sasa itamenyana na Uingereza siku ya Jumapili.

Kikosi hicho kinachoitwa kwa jina maarufu la Shujaa, kilianza vema kutetea taji lake baada ya kushinda mechi ya ufunguzi kwa kuwalemea Argentina,kwa  alama 22-7 lakini ikakubali kichapo cha Australia cha alama 29-7.

Timu zingine ambazo zimefuzu katika hatua ya robo fainali ni pamoja na mabingwa michezo ya Olimpiki Fiji.

Canada nayo imefuzu kutoka kundi A, sawa na Ungereza huku New Zealand na Marekani nazo zikijikatia tiketi katika kundi D.

Nahodha wa Kenya Andrew Amonde amesema lengo lao ni kushinda tena taji hili.

Mashindano ya msimu huu yalianza mwezi Desemba mwaka uliipita, na tayari Afrika Kusini imeshinda mataji manne mwezi Desemba mwaka jana pamoja na Januari, Februari na Machi mwaka huu.

Uingereza wameshinda mbara mbili, mwezi  Desemba mwaka uliopita na mwezi Machi mwaka huu, huku Fiji ikishinda mapema mwezi huu wa Aprili.

Mashindano haya yatamalizika mwisho wa mwezi wa Mei jijini London nchini Uingereza lakini kabla ya hapo, kutakuwa na michuano mingine jijini Paris nchini Ufaransa mapema mwezi Mei.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana