Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Marekani, Canada na Mexico kuomba kuandaa kwa pamoja fainali za mwaka 2026

media The snow-covered landscape is reflected in a logo in front of FIFA headquarters in Zurich, Switzerland, January 10, 2017. REUTERS/Arnd Wiegmann/Files

Marekani, Canada na Mexico zimetangaza kuwa zitaomba kwa pamoja kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2026.

Ikiwa nchi hizi zitaomba kwa pamoja, itakuwa ni mara ya kwanza baada ya kuongezwa kwa timu kutoka 32 hadi timu 48 na ikiwa zitafanikiwa kushinda kuandaa itakuwa ni mara ya kwanza pia kwa fainali hizi kuandaliwa na nchi tatu.

Mapendekezo ya nchi hizi itakuwa ni kwa Marekani kuandaa mechi 60 huku mechi 10 zikiandaliwa kwa pamoja na nchi za Canada na Mexico.

Uamuzi wa nani ataandaa fainali za mwaka 2026 utatangazwa ifikapo mwaka 2020.

Hii itakuwa ni miaka mitatu baadae kuliko ambavyo ni kawaida kutokana na tuhuma za rushwa zilizoibuka wakati wa utolewaji wa zabuniya kuandaa fainali za mwaka 2018 na 2022 nchini Urusu na Qatar.

Marekani iliandaa fainali za kombe la dunia mwaka 1994 ambazo zilitajwa kuwa na wahudhuriaji wa wastani katika historia ya michuano ya kombela dunia, huku nchi ya Mexico ikiwa ni nchi ya kwanza kuandaa fainali hizi mara mbili kwenye mwaka 1970 na 1986 na Canada yenyewe iliandaa fainali za kombe la dunia za wanawake mwaka 2015.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa atajenga ukuta kutenganisha nchi yake na Mexico, lakini rais wa shirikisho la soka nchini Marekani Sunil Gulat amesema Trump anaunga mkono ombi la kuandaa fainali hizo na ametutaka tufanye hivyo.

Gulat amesema nchi yake ile ya Canada na Mexico kwa pamoja zimeeleza nia yao ya dhati kabisa ya kuandaa fainali hizo.

Gulati amesema ikiwa nchi hizo zitakuja pamoja na kuandaa fainali za mwaka 2026, hakuna shaka kuwa Marekani, Canada na Mexico zitaandaa fainali za aina yake.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana