Pata taarifa kuu
AFCON 2019

Madagascar yafuzu hatua ya makundi kutafuta tiketi ya AFCON 2019

Timu ya taifa ya soka ya Madagascar maarufu kama Barea, kwa mara nyingine imepata nafasi ya kufuzu kucheza mechi za kuelekea katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.

Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF
Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF Cafonline
Matangazo ya kibiashara

Madagascar imefuzu kucheza katika hatua ya makundi baada kuishinda Sao- Tome kwa jumla ya mabao 4-2 katika mchuano wa nyumbani na ugenini katika hatua ya awali.

Madagascar sasa itakuwa mbioni kutafuta kushinda kundi hilo dhidi ya Senegal, Equitorial Guinea na Sudan.

Madagascar haijawahi kufuzu katika michuano ya fainali ya bara Afrika katika historia ya mchezo wa soka.

Hata hivyo, nchi hiyo imewahi kuishinda Misri bao 1-0 katika mchuano muhimu wa kufuzu kucheza fainali ya mwaka 2004 nchini Tunisia.

Mwaka 2016, Madagascar ilishindwa kufuzu kwenda nchini Gabon baada ya kufungwa mechi zake zote za kufuzu dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na DR Congo.

Madagascar ilicheza mechi yake ya kwanza ya Kimataifa dhidi ya Mauritius mabao 2-1 mwaka 1947.

Ushindi mkubwa ambao imewahi kupata ni dhidi ya Congo mabao 8-1 mwaka 1960.

Kikosi cha sasa cha Madagascar:-

Makipa: Eddit Bastia (Elgeco Plus), Ibrahim Dabo (US Creteil Lusitanos, Ufaransa).

Mabeki : Mario Bakary (Fosa Juniors), Tobisoa Njakanirina (CNaPS Sports), Toavina Rambeloson (US Tourcoing, Ufaransa), Tantely Randrianiaina (CNaPS Sports), Pascal Razakanantenaina (Arras, Ufaransa.

Viungo wa Kati: Arohasina Andrianarimanana, Jean Claude Marobe (both Fosa Juniors), Jean Stéphane Raheriharimanana (Red Star, Ufaransa), Ferdinand Ramanamahefa (RC Flechols, Ufaransa), Zotsara Randriambololona (RE Virton, Ubelgiji), Mirija Rasoanaivoarison (CNaPS Sports)

Washambuliaji: Carolus Andriamahitsinoro (USM Alger, Algeria), Faneva Andriantsima (Sochaux, Ufaransa), Rinjala Raherinaivo (FC Sion, Uswizi), Paulin Voavy (Makassa, Misri).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.