Pata taarifa kuu
RIADHA

Kenya yapata medali ya dhahabu katika mbio maalum ya Kilomita nane

Kenya imeshinda medali ya kwanza ya dhahabu katika mashidano mapya ya riadha ya kupokezana kitambaa baina ya wanariadha wa kiume na kike katika mashindano ya dunia ya nyika yaliyofanyika siku ya Jumapili katika uwanja wa Kololo jijini Kampala nchini Uganda.

Wanariadha wa Kenya baada ya kushinda taji la mbio za kupokezana kitambaa katika mashindano ya riadha  nyika ya dunia yaliyofanyika Jumapili Machi 26 2017 jijini Kampala
Wanariadha wa Kenya baada ya kushinda taji la mbio za kupokezana kitambaa katika mashindano ya riadha nyika ya dunia yaliyofanyika Jumapili Machi 26 2017 jijini Kampala www.iaaf.org
Matangazo ya kibiashara

Wanariadha wa Kenya waliongozwa na mkongwe na bingwa mara tatu wa mashindano ya dunia na Olimpiki katika mbio za Mita 1500 Asbel Kiprop.

Wanariadha wengine waliokimbia pamoja na Kiprop ni Winfred Mbithe, Bernard Koros na Beatrice Chepkoech.

Ushindi huu umeifanya Kenya kuweka historia ya kupata medali ya dhahabu katika mbio hizo za Kilomita nane ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano haya.

Kila mwanariadha alikimbia Kilomita mbili na kumpa mwezake kitambaa hadi mizunguko yote ya Kilomita nane zilipomalizika.

Ushindi wa Kenya umewapa Dola za Marekani elfu 12 kutoka kwa Shirikisho la mchezo wa riadha duniani IAAF, huku washindi wa pili hadi wanne wakigawana Dola elfu 18.

Wanariadha wa Ethiopia wakiongozwa na bingwa wa dunia wa mbio za Mita 1500 Genzebe Dibaba, walimaliza katika nafasi ya pili, akiwa na wanariadha wenzake Welde Tufa, Bone Cheluke na Yomif Kejelcha.

Uturuki walichukua nafasi ya tatu, Uganda nao wakifunga nne bora.

Tanzania iliyowakilishwa na wanariadha Faraja Damas Lazaro, Sicilia Panga, Jackline Sakilu na Marco Silvester Monko walimaliza katika nafasi ya nane kati ya mataifa 13 yaliyoshiriki, huku Sudan Kusini ikiwa ya mwisho.

Mbio hizi ziliwashirikisha wanariadha wengi wanaoshiriki mbio za kati za Mita 1500, 3000 na 800.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.