Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

TP Mazembe yamfuta kazi kocha wake kwa matokeo mabaya

media Kocha Thierry Froger Wikipedia

Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imemfuta kazi kocha wake Thierry Froger.

Hatua hii inakuja chini ya miezi miwili baada ya kupewa kibarua cha kuifunza klabu hiyo kwa muda wa mwaka mmoja.

Uongozi wa klabu hiyo umesema baada ya matokeo mabaya katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika msimu huu, wameelewana na raia huyo wa Ufaransa kusitisha mkataba wake.

Mazembe ambao ni mabingwa mara tano wa taji hilo, waliondolewa katika michuano ya mwaka huu na CAPS United ya Zimbabwe kwa faida ya bao la ugenini baada ya mchuano wa marudiano kutoka sare ya 0-0 baada ya sare nyingine ya 1-1 katika mchuano wa kwanza mjini Lubumbashi.

Thierry, mwenye umri wa miaka 53 alichukua nafasi ya Mfaransa mwenzake Hubert Velud ambaye alijiuzulu baada ya kuisaidia TP Mazembe kunyakua taji la Shirikisho barani Afrika mwaka 2016.

Baada ya kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa, Mazembe sasa itaendelea kushiriki katika michuano ya kuwania taji la Shirikisho ambalo wao ndio mabingwa watetezi.

Klabu hiyo imepangwa kucheza na JS Kabylie ya Algeria katika hatua ya mwondoano, mechi zitakazopigwa mwezi Aprili na mshindi kufuzu katika hatua ya makundi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana