Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-UCHAGUZi

Gianni Infantino: Niko tayari kufanya kazi na Ahmad

Rais wa Shirikisho Kimataifa la Soka (FIFA), Gianni Infantino amekaribisha ushindi wa Ahmad katika uchaguzi wa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Rais wa FIFA amepongeza kazi ya Issa Hayatou na alikanusha kuwa habari zinazosema kuwa alichangia kwa kumuangusha Issa Hayatou baada ya miaka 29 akiiongoza CAF.

Le prΓ©sident de la FIFA, Gianni Infantino.
Le prΓ©sident de la FIFA, Gianni Infantino. Reuters / Matthew Childs
Matangazo ya kibiashara

Akiulizwa kuhusu anachofikiria kuhusu matokeo ya uchaguzi huu wa urais wa Shirikisho la Soka Afrika, Gianni Infantino alijibu akisem akuwa ilikua ni dsiku muhimu kwa CAF.

"Huu ni mchakato wa kidemokrasia unaotaka hivyo. Kwanza tungempongeza Ahmad ambaye amechaguliwa. Pia tunatakiwa kumshukuru na kufikisha pongezi zetu za dhati kwa Bw Hayatoukwa yale yote aliyofanya katika miaka yake 29 kama Rais wa CAF, " Bw Infantino amesema.

Gianni Infantino amebaini kwamba miaka ishirini na tisa aliyoongoza Issa Hayatou ni muda mrefu. Hata hivyo amesema kuwa ni maamuzi ya Mkutano Mkuu wa CAF ambayo pia yalimfanya rais Hayatou kuhaguliwa tena mara kadhaa.

"Alifanya kazi yake, aliendeleza Afrika. Na sasa kumekua na mabadiliko. Lakini hakuna cha kushangaza, " ameongeza Gianni Infantino.

Akiulizwa na RFI iwapo anamjua rais mpya wa CAF na kuwa yuko tayari kushirikiana naye, Bw Infantino amesema yuko tayari kufanya kazi na rais mpya wa CAF.
" Namjua kwa kipindi fulani hivi. Ni shabiki wa soka. Anafanya kazi kwa bidii katika soka. Nina uhakika atajiunga vizuri katika timu yetu, " amesem arais wa FIFA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.