Pata taarifa kuu
UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Arsenal itaweza kubadili matokeo dhidi ya Bayern Minich, Real nao kiwanjani

Mechi za mtoano za raundi ya pili ya michuano ya klabu bingwa Ulaya zitapigwa tena Jumanne ya wiki hii, ambapo kutakuwa na mechi mbili pekee, huku klabu ya Arsenal ya Uingereza ikisubiriwa kuona ikiwa itafanya maajabu dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani. 

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akisalimia na mchezaji wake Alexis Sanchez anayeripotiwa kutofautiana na kocha wake. Machi 6, 2017
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akisalimia na mchezaji wake Alexis Sanchez anayeripotiwa kutofautiana na kocha wake. Machi 6, 2017 Reuters / John Sibley Livepic
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha Arsene Wenger kitakuwa nyumbani kwenye dimba lake la Emirates kuwakaribisha mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani Bayern Minich ambao wanasafiri jijini London wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 5-1 iliyoupata kwenye mchezo wa awali.

Arsenal wataingia uwanjani wakiwa na lengo moja tu la kujaribu kupindua matokeo ya Ujerumani, jambo ambalo licha ya kuwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu linawezekana, lakini wachambuzi wa soka wanaona itakuwa ni vigumu sana kwa Arsenal kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Beyern.

Ikiwa Arsenal watataka kusinga mbele kucheza hatua ya robo fainali, watahitaji kupata ushindi wa mabao 4-0, jambo ambalo kocha Arsene Wenger bado anasema linawezekana.

Mchezo mwingine utazikutanisha timu ya Napoli ambayo itakuwa nyumbani kuwakaribisha vinara wa ligi ya Uhispania, Real Madrid, katika mchezo mwingine ambao unasubiriwa kwa hamu na gamu.

Kwenye mchezo wa awali ambao Madrid walikuwa nyumbani, walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 3-1.

Hivi leo Napoli watakuwa nyumbani kuwakaribisha Real Madrid huku wakijua fika kuwa wanahitaji angalau kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Madrid ama kupata mabao zaidi.

Mechi zote hizi zitapigwa majira ya saa nne na dakika arobaini na tano kwa saa za hapa Afrika Mashariki (22:45pm EAT).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.