Pata taarifa kuu
FIFA

Fifa yamfungua kwa miaka miwili aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji, Amos Adamu

Mjumbe wa zamani wa kamati ya utendaji ya shirikisho la kabumbu duniani Fifa, raia wa Nigeria, Amos Adamu, amefungiwa kujihusisha na masuala yoyote ya soka kwa kipindi cha miaka miwili, imesema taarifa ya Fifa.

Nembo ya Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) mbele ya shirikisho hilo mjini Zuric Oktoba 8, 2015.
Nembo ya Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) mbele ya shirikisho hilo mjini Zuric Oktoba 8, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la kabumbu duniani Fifa, kwenye taarifa yake limesema kuwa, adhabu hii imeanza kutekelezwa rasmi tarehe 28 Februari 2017.

Adamu ambaye awali tayari alishaadhibiwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miaka mitatu mwaka 2010, ameadhibiwa tena kwa makosa ya kukiuka sheria za maadili za shirikisho la mpira Fifa.

Kiongozi huyu mwenye umri wa miaka 64 hivi sasa, amekutwa na hatia ya kukiuka sheria za ujumla za Fifa, mirabaha na kuwa na mgongano wa kimaslahi kwenye baadhi ya mambo ya shirikisho hilo.

Taarifa ya Fifa imesema kuwa, makosa yake yanahusiana na ushiriki wake wakati wa maandalizi wa fainali za kombe la dunia mwaka 2010 wakati yeye akiwa kama mjumbe wa kamati ya utendaji ya Fifa ya wakati huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.