Pata taarifa kuu
MAN UTD

Mourinho awataka wachezaji wake wasibweteke na badala yake kushinda mataji zaidi

Saa chache baada ya kushuhudia timu yake ikitwaa taji la kombe la ligi nchini Uingereza, kocha mkuu wa klabu ya Manchester United, mreno Jose Mourinho, amewapa changamoto wachezaji wake kutumia ushindi wao wa siku ya Jumapili, kushinda mataji makubwa zaidi.

Wachezaji wa klabu ya Manchester United wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe cha ligi, walichoshinda jana dhidi ya Southampton.
Wachezaji wa klabu ya Manchester United wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe cha ligi, walichoshinda jana dhidi ya Southampton. Reuters / Carl Recine Livepic
Matangazo ya kibiashara

Mourinho ambaye siku ya Jumapili ya Februari 26 alinyakua taji lake la kwanza akiwa na klabu ya Manchester United baada ya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic kuipatia timu yake bao la ushindi katika dakika za lala salama.

United waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika mchezo ambao kwa sehemu kubwa ulitawaliwa na klabu ya Southampton.

Mourinho anakuwa kocha wa kwanza kushinda taji na timu hiyo katika msimu wa kwanza wa ligi toka alipochukua nafasi hiyo, ikiwa ni taji lake la 19 katika historia yake ya maisha ya ufundishaji soka.

Hata hivyo kocha huyu mwenye umri wa miaka 54 hivi sasa, anawataka wachezaji kujifunza kutokana na ushindi walioupata wakati huu wakifukuzia kushinda taji la FA na lile la Europa League ambayo wamesalia katika mashindano hayo.

"Ukweli ni kwamba tunahitaji mafanikio zaidi, mkataba wangu ni mrefu, nina miaka miwili zaidi ikiwemo huu, kwahivyo natumaini nitashinda mataji zaidi.

Licha ya ushindi huu, Mourinho baada ya mechi hakuonekana kuwa mwenye furaha hata baadaya kukabidhiwa kushika kombe ililoshinda timu yake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.