Pata taarifa kuu
AFCON 2017

Uganda yamaliza michuano ya AFCON kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mali

Uganda imeondoka katika michuano ya soka ya mataifa bingwa barani Afrika kwa tabasamu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mali katika mchuano wake wa mwisho wa kundi D. 

Mashabiki wa Uganda wakishabikia timu yao ya taifa.
Mashabiki wa Uganda wakishabikia timu yao ya taifa. RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Mchuano huo ulichezwa siku ya Jumatano katika uwanja wa Stade d'Oyem, mjini Oyem.

Uganda Cranes ilicheza mchuano huo wa mwisho kwa kujiamini na ilianza kwa kupata bao katika dakika ya 70 kupitia mshambuliaji matata Farouk Miya katika dakika ya 70 ya mchuano huo.

Hata hivyo, dakika tatu baadaye baada ya Uganda kuwa kifua mbele, Mali ilitoka nyuma na kusawazisha kupitia Yves Bissouma katika dakika ya 73 ya mchuano huo.

Uganda Cranes inarejea jijini Kampala ikiwa na historia ya michuano hii kwa kupata sare moja na kufungwa bao 1-0 na Ghana na Misri.

Kocha Milutin Micho ambaye alikuwa analenga kufika katika hatua ya robo fainali baada ya Uganda kurejea katika michuano hii kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978, amesema Uganda imejifunza mambo mengi katika michuano hii.

Mbali na mchuano huo, Misri nayo ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Ghana katika uwanja wa Port-Gentil.

Bao pekee la Misri lilifungwa na Mohammed Salah katika dakika 11 ya mchuano huo.

Uganda imemaliza kundi hilo kwa alama alama 7, ikifuatwa na Ghana ambayo ina alama 6. Mataifa haya yamefuzu katika hatua ya robo fainali.

Michuano ya robo fainali:

Januari 28 2017
Burkina Faso vs Tunisia-Mechi itachezwa mjini Libreville.
Senegal vs Cameroon-Mechi itachezwamjini Franceville.

Januari 29 2017
Misri vs Morocco-Mech itachezwa mjini Port Gentil.
DR Congo vs Ghana-Mechi itachezwa mjini Oyem.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.