Pata taarifa kuu
SOKA-AFCON 2017

Viwanja vyasalia vitupu katika michuano ya AFCON nchini Gabon

Michuano ya soka kutafuta ubingwa wa Afrika inavyokaribia kuingia katika hatua ya robo fainali nchini Gabon, idadi ya mashabiki wanaojitokeza kushuhudia michuano hii inaendelea kupungua.

Uwanja wa Kimataifa wa  'Amitié jijini  Libreville.
Uwanja wa Kimataifa wa 'Amitié jijini Libreville. RFI/Marco Martins
Matangazo ya kibiashara

Huenda hali ikawa mbaya zaidi hasa baada ya wenyeji Gabon kuondolewa katika michuano hii wiki hii.

Michuano hii inachezwa katika viwanja vya Amitie jijini Libreville, Franceville, Oyem na Port-Gentil.

Wingi wa mashabiki ulionekana wakati wa michuano ya wenyeji Gabon katika uwanja wa Stade de l'Amitie jijini Libreville, ulio na uwezo wa kuwaingiza mashabiki 40,000.

Pamoja na Shirikisho la soka barani Afrika CAF  kubaini hilo na kupunguza kiingilio cha kuingia uwanjani kutoka Franca 500 hadi 70, na hata serikali kujitolea kuwalipia baadhi ya mashabiki, viwanja vimesalia vitupu.

Mfano mzuri ni wakati wa mchuano kati ya Algeria na Tunisia ambapo kulikuwepo kwa mashabiki 1,000 katika uwanja wa Franceville ulio na uwezo wa kuwaingiza mashabiki 22,000.

Mvutano wa kisiasa kati ya rais Ali Bongo na mpinzani wake Jean Ping kwa kiasi fulani unaelezwa kusababisha uchache wa mashabiki kutofika uwanjani kwa wingi, baada ya mwanasiasa huyo kuwaambia wafuasi wake kususia michuano hii.

Michuano hii inaendelea wakati huu ligi kuu za soka nchini Ulaya zikiendelea hasa nchini Uingereza.

Mashabiki wengi wamejikuta wakiangalia michuano ya soka barani Ulaya kupitia runinga na kusahau mechi za nyumbani.

Pamoja na hilo, raia wa Gabon wameamua kuangalia michuano hiyo kupitia runinga badala ya kwenda uwanjani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.