Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Gabon yaingia katika historia mbaya ya wenyeji wa michuano ya AFCON

media Wachezaji wa Gabon wakiingia uwanjani kumenyana na Cameroon katika mchuano wa mwisho wa kundi A Januari 22 2017 ©Pierre René-Worms

Timu ya taifa ya soka ya Gabon, imeingia katika historia ya kuwa mojawapo ya mataifa manne wenyeji ambayo yamewahi kuondolewa katika hatua ya makundi katika harakati za kuwania taji la soka barani Afrika.

Safari ya Gabon ilifika mwisho, Jumapili ya wiki iliyopita baada ya kutoka sare ya 0-0 na Cameroon.

Mashabiki wa Gabon waliofurika kwa maelfu katika uwanja wa Amitie, jijini Libreville kushabikia timu yao wamevunja mioyo na hatua hii.

Kuna hofu kubwa kuwa baada ya Gabon kuondolewa, huenda idadi ya mashabiki wanaohudhuria michuano hii ikapungua hata.

Katika michuano hii, Gabon ilitoka sare ya bao 1-1 na Guinea Bissau lakini pia ikaandikisha matokeo kama hayo dhidi ya Burkina Faso.

Tunisia

Mbali na Gabon, mwaka 1994 Tunisia ilijipata katika nafasi hiyo baada ya kumaliza ya mwisho katika kundi lao lililokuwa na Zaire na Mali.

Tunisia ilifungwa na Mali mabao 2-0 na baadaye kutoka sare na Zaire sare ya bao 1-1.

Mwaka huo, Nigeria ilishinda taji hilo.

Ivory Coast

Mwaka 1984, The Elephants wakiwa wenyeji walijipata wakiondoka mapema katika michuano hi baada ya kulemewa na Misri, Cameroon na Togo.

Ilimaliza katika nafasi ya tatu katika kundi hilo kwa alama mbili baada ya kufungwa na Misri mabao 2-1 na Cameroon 2-0.

Cameroon ndio walikuwa mabingwa.

Ethiopia

Mwaka 1976, Ethiopia ilikuwa mwenyeji wa michuano hii.

Ilijikuta ikiyaaga mashindano haya baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi lake lililokuwa na Guinea, Misri na Uganda.

Mwaka huo, Ethiopia ilifungwa na Guinea mabao 2-1 na baadaye kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Misri.
 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana