Pata taarifa kuu
AFCON 2017-GABON

Afcon 2017: Mzunguko wa pili katika hatua ya makundi kuanza

Mechi za mchezo wa soka mzunguko wa pili hatua ya makundi kutafuta ubingwa wa bara Afrika, zinaanza kuchezwa Jumatano hii nchini Gabon.

Mashabiki wa Gabon na Cameroon wakiangalia mchuano wa kwanza wa Afcon 2017 uliozikutanisha timu ya taifa ya Gabon dhidi ya Guinea Bissau, Januari 14, 2017.
Mashabiki wa Gabon na Cameroon wakiangalia mchuano wa kwanza wa Afcon 2017 uliozikutanisha timu ya taifa ya Gabon dhidi ya Guinea Bissau, Januari 14, 2017. ©Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Wenyeji Gabon wanarejea tena katika uwanja wa Amitie, jijini Libreville kumenyana na Burkina Faso.

Mechi hii itachezwa kuanzia saa moja kamili jioni saa za Afrika Mashariki, chini ya refarii kutoka Gambia Bakary Gasssama.

Gabon inatumai kuwa itaandikisha ushindi leo, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu katika mzunguko wa pili na kuwafurahisha mashabiki wa nyumbani.

Baadaye, Cameroon itachuana na Guinea-Bissau inayoshiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza.

Uchambuzi wa kina

Hadi sasa, ni mataifa matatu kati ya 16 yanayoshiriki katika michuano hii ambayo yamepata ushindi katika mzunguko wa kwanza.

Mataifa yaliyopata ushindi ni pamoja na Senegal iliyoifunga Tunisia mabao 2-0 na sasa inaongoza kundi la B kwa alama tatu, mbele ya Algeria, Zimbabwe na Tunisia.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nayo ilianza vema baada ya kuishinda Morocco kwa bao 1-0.

Leopard ndio timu pekee iliyopata ushindi katika kundi la C.

Ghana pia ni timu nyingine, ambayo imefanikiwa kupata ushindi katika mzunguko wa kwanza.

Siku ya Jumanne usiku, iliishinda Uganda bao 1-0 mjini Port-Gentil katika mchuano wa kundi D.

Matokeo ya sare katika makundi yote

Kundi A

Gabon 1-1 Guinea-Bissau
Burkina Faso 1-1 Cameroon

Kundi B

Algeria 2-2 Zimbabwe

Kundi C

Cote d'Ivoire 0-0 Togo

 Mali 0-0 Misri

Wachambuzi wa soka wanasema sare hii inamaanisha kuwa kuna ushindani mkali sana katika makala haya 31 ya Afcon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.