Pata taarifa kuu
AFCON 2017-GABON-GHANA-UGANDA

Afcon 2017: Ghana yaiadhibu Uganda

Timu ya taifa ya Ghana, iliyotwaa kombe katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka juzi, imeanza michuano hii Afcon 2017 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda, Jumanne hii Januari 17 katika uwanja wa Port-Gentil. Mkwaju wa Penalti uliowekwa wafuni na Andre Ayew umeipa furaha ya kutosha Black Stars katika kundi D.

Kiungo wa kati wa Ghana, Andre Ayew, ambaye amefunga katika mechi ya timu yake dhidi ya Uganda, Januari 17, 2017.
Kiungo wa kati wa Ghana, Andre Ayew, ambaye amefunga katika mechi ya timu yake dhidi ya Uganda, Januari 17, 2017. Pierre René-Worms / RFI
Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Uganda, moja ya timu ambazo hazina umaarufu katika michuano hii ya Afcon huu 2017, washindwa kuiga utaratibu uliotumiwa na timu ya taifa ya Guinea-Bissau na Zimbabwe. Uganda haikufaulu kubadili matokeo ya mchezo hadi dakika tisini.

"Cranes ingelijitahidi hata hivyo kutoka sare, kama walivyofanya Guinea Bissau dhidi ya Gabon au Zimbabwe dhidi ya Algeria.

Lakini Ghana, mshindi wa micuno ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka juzi, ilitumia ujuzi wake na ukakamavu wa wachezaji wake ili kupata ushindi huo.

Ghana yaanza vizuri Afcon 2017

Bao la Ghana lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Andre Ayew, katika dakika ya 30 ya mchezo. Kiungo huyo wa kati wa Ghana alimfunga Denis Onyango, kipa wa Uganda, ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa mchezaji bora anayechezea barani Afrika.

Onyango na wenzake watajaribu kufanya vizuri katika mechi yao dhidi ya Misri, Jumamosi, Januari 21 kwenye uwanja wa Port-Gentil. "Black Stars" ya Ghana, watamenyana na Mali ndani ya siku nne zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.