Pata taarifa kuu
AFCON 2017-GABON

Gabon yatoka sare dhidi ya Guinea Bissau katika mechi ya ufunguzi ya AFCON

Michuano ya 31 ya Kombe la Mataifa ya Afrika hatimaye yamezinduaJumamosi hii Januari 14, 2017. Kwa mechi hii ya uzinduzi wa AFCON 2017, Gabon na Guinea-Bissau wamejitupa uwanjani.

Mshambulizi wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang (katikati) akiwa na furaha baada ya bao lake dhidi ya Guinea-Bissau katika mechi ya ufunguzi wa CAN 2017, Januari 14, 2017 katika Uwanja wa Amitie mjini Libreville.
Mshambulizi wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang (katikati) akiwa na furaha baada ya bao lake dhidi ya Guinea-Bissau katika mechi ya ufunguzi wa CAN 2017, Januari 14, 2017 katika Uwanja wa Amitie mjini Libreville. RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Hadi dakika kipenga cha mwisho timu hizi mbili zilijikuta zikitoka sare ya kufungana bao 1-1. Huu ni mchuano wa kwanza ambao haujatoa ushindi kati ya timu zote mbili.

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo timu zote mbili zilijikuta zinatoka sare ya kutofungana. Na katika dakika ya 8 ya kipindi cha pili mchezaji nyota wa Borussia Dortmund, Pierre Emerick-Aubameyang alichezesha nyavu za Guinea Bisau kwa kupachika bao la kwanza.

Licha Gabon kutawala mpira katika kipindi cha kwanza na katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili, Guinea-Bissau ilikuja juu na kusawazisha kupitia beki wake Juary Soares baada ya kupewa pasi ya mbali na Zezinho.

Wachezaji wa Guinea Bissau wakifurahia bao lao la kusawazisha dhidi ya Gabon.
Wachezaji wa Guinea Bissau wakifurahia bao lao la kusawazisha dhidi ya Gabon. RFI/Pierre René-Worms

Itafahamika kwamba ni kwa mara ya kwanza Guinea-Bissau inashiriki michuano hii ya Kombe la Afrika.

Katika kipindi cha siku 23 timu 16 zitachuana kuwania kombe hilo lenye umaarufu mkubwa barani.

Mechi hizo zilitarajiwa kufanyika nchini Libya ,lakini vita vya wenyewe kwa wenyewe viliwalazimu wasimamizi kubadili nia na kuelekea Gabon ambayo iliandaa michuano hiyo mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.