Pata taarifa kuu
AFCON 2017

Mataifa matano yatakayokosa AFCON 2017 nchini Gabon

Makala ya 31 ya michuano ya soka kuwania taji la bara Afrika, inayofungua milango yake siku ya Jumamosi nchini Gabon.

Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF
Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF cafoline
Matangazo ya kibiashara

Mchuano wa ufunguzi utakuwa kati ya Gabon na Guinea Bissau.

Hata hivyo, tunakuletea mataifa matano ambayo yameshindwa kufuzu katika michuano hii.

Nigeria

Super Eagles ilishindwa kufuzu katika michuano hii baada ya kufanya vibaya katika michuano ya kujikatia tiketi.

Katika kundi lao, ilipata alama moja na kuipa Misri nafasi ya kufuzu katika michuano hii.

Hii ni mara ya tatu kwa mabingwa hao ambao wameshinda taji hili mara tatu, kufuzu katika michuano hii.

Cape Verde
Taifa hili hili dogo la watu 500,000, nalo lililemewa katika kundi lake hasa baada ya kufungwa na Libya nyumbani.

Cape Verde ilihitaji ushindi dhidi ya Libya ili kufuzu kwenda Gabon lakini matumaini yalididimia baada ya kufungwa bao 1-0 nyumbani.

Taifa hili ambalo limeonekana kuimarika katika miaka ya hivi karibuni, mara ya mwisho kucheza katika fainali za AFCON ilikuwa ni mwaka 2013 nchini Afrika Kusini na 2015 nchini Equitorial Guinea.

Congo Brazzaville
Ilifika katika hatua ya robo fainali wakati michuano hii ilipofanyika mwaka 2015 nchini Equitorial Guinea.

Red Devils kama inavyofahamika, ilishindwa kufuzu baada ya kufungwa na Harambee Stars ya Kenya na kuwanyima alama muhimu.

Afrika Kusini
Bafana Bafana ilishindwa kufuzu baada ya kuanza katika michuano yake.

Ilitoka sare na Gambia na baadaye kufungwa na Mauritania , matokeo ambayo iliwanyima nafasi ya kufuzu.

Ilimaliza nafasi ya tatu katika kundi lao baada ya kupata ushindi mmoja.

Zambia
Mabingwa wa mwaka 2012, nao walishindwa kufuzu baada ya kupata ushindi mmoja tu kati ya michuano sita ya kufuzu.

Ilimaliza ya tatu nyuma ya Guinea-Bissau na Congo Brazaville.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.