Pata taarifa kuu
CHELSEA-TOTTENHAM-EPL

Mwiko wa Chelsea wa kutopoteza michezo 13 mfululizo wavunjwa na Tottenham

Kiungo wa Tottenham aliyeko kwenye kiwango cha juu hivi sasa, Dele Alli, aliifungia timu yake mabao mawili na kufanikiwa kuwafunga vinara wa ligi hiyo klabu ya Chelsea, na kuzima matumaini ya timu hiyo kufikisha mchezo wa 14 bila kupoteza. 

Kiungo wa Tottenham Hotspurs, Dele Alli, akiifungua timu yake bao la pili kwa kichwa, Januari 4, 2017
Kiungo wa Tottenham Hotspurs, Dele Alli, akiifungua timu yake bao la pili kwa kichwa, Januari 4, 2017 Reuters / Andrew Couldridge Livepic
Matangazo ya kibiashara

Timu ya Chelsea, ilikuwa ikijaribu kuwa timu ya kwanza kupata ushindi katika michezo 14 mfululizo na kusalia kwenye uongozi wa ligi kuu ya Uingereza, lakini mabao ya Dele Alli yaliyotengenezwa kwa pasi nzuri za mchezaji Christian Eriksen yalitosha kuzamisha jahazi la kocha Antonio Conte.

"Tulikuwa tunashindana na moja ya timu iliyobora kabisa, klabu bora Ulaya, na tunajisikia vizuri na kwakweli tulicheza kwa kiwango kikubwa," alisema kocha wa Spurs Mauricio Pochettino.

Kikosi cha Antonio Conte kilikuwa kinataka kuweka rekodi kwa kushinda mchezo wa 14 mfululizo wakati huu tayari akiwa amefikia rekodi ya Arsenal ya kushinda mechi 13 mfululizo katika msimu wa mwaka 2001-2002 na sasa wanabakiza alama tano pekee mbele ya Liverpool.

Hata hivyo kuvunjwa kwa rekodi yao ya ushindi mfululizo, kumetoa matumaini kwa vilabu vingine kuwa na nafasi ya kushinda taji la ligi kuu ya nchi hiyo, wakiwemo Tottenham wenyewe, Manchester City, Arsenal na Manchester United.

"Ni bahati mbaya sana rekodi yetu kusimamishwa, lakini Tottenham ni timu nzuri, ni timu ngumu na nafikiri kabisa kuwa inaweza kupambana kutwaa taji kama itafanya hivi hadi mwisho wa msimu." alisema kocha Conte.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.