Pata taarifa kuu
CHELSEA-UFARANSA

Mashabiki 4 wa Chelsea waliotoa matamshi ya kibaguzi wakabiliwa na kifungo Paris

Mashabiki wa nne wa klabu ya Chelsea ya Uingereza, akiwemo polisi mmoja, wanakabiliwa na kesi ya ubaguzi katika mahakama ya jijini Paris, Ufaransa, ambapo huenda wakakabiliwa na kifungo.

Wafanyakazi wa Uefa wakitandaza uwanjani moja ya bango la shirikisho la mpira Ulaya
Wafanyakazi wa Uefa wakitandaza uwanjani moja ya bango la shirikisho la mpira Ulaya REUTERS/Regis Duvignau Livepic
Matangazo ya kibiashara

Wakiwa ndani ya gari moshi, mashabiki hao wanne wa Chelsea walikuwa miongoni mwa kundi la mashabiki waliokuwa wakitamka maneno ya kibaguzi wakidai "sisi ni wabaguzi, na hivyo ndivyo tunavyopenda" wakati huo walikuwa wakimsukuma nje ya gari moshi abiria mmoja mwenye asili ya Afrika.

Wakiwa mahakamani, mashabiki hao walikana mashtaka wakidai kuwa maneno waliyotoa hayakuwa na asili ya ubaguzi.

Joshua Parsons, umri miaka 22 na mwanafunzi wa zamani katika shule ya Millfield nchini Uingereza, huku James Fairbairn, 25, yeye akiwa ni mhandisi walikuwa ni miongoni mwa waliopandishwa kizimbani.

Richard Barklie, umri miaka 52 na polisi mstaafu, sambamba na William Simpson, mwenye umri wa miaka 27, walishtakiwa huku wakiwa hawapo mahakamani.

Tukio hili la mwezi Februari mwaka 2015, lilikuwa kabla ya mchezo wa klabu bingwa Ulaya kati ya Chelsea na PSG, na mashabiki hao wa Chelsea walipigwa picha na Muingereza Paul Nolan ambaye aliichapisha kwenye gazeti la Guardian.

Katika video hiyo iliyooneshwa mahakamani, inamuonesha abiria Souleymane Sylla, akijaribu bila mafanikio kuingia ndani ya gari moshi lakini mashabiki hao walimsukuma.

Tayari mashabiki, Parsons, Fairbairn na Barklie wameshapewa adhabu nchini Uinhereza ya kutoingia uwanjani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.