sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mazungumzo ya amani kuanza Sudan, rais …
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania John Magufuli. 13 Juni 2019
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Ligi kuu ya soka nchini DRC yasitishwa

media Nembo ya Shirikisho la soka nchini DRC FECOFA

Waziri wa Michezo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Denis Kambayi ametangaza kusitisha ligi kuu ya soka nchini humo hadi tarehe 14 mwezi Januari mwaka 2017.

Kambayi amesema, serikali imechukua uamuzi huo kutokana na ongezeko la vurugu katika viwanja vya soka na ukosefu wa uaminifu katika ukusanyaji wa mapato wakati kuna mechi uwanjani katika siku za hivi karibuni lakini pia kwa sababu za kisiasa.

Aidha, Waziri huyo amesema kutokarabatiwa kwa vifaa muhimu uwanjani na tabia mbaya ya mashabiki ya kupigana na kuzozana wanapokuwa uwanjani, kumesababisha hatua hii kufikiwa.

Waziri Kambayi amesema atakutana na viongozi wa soka nchini humo kuona namna ya kutatua changamoto hii kabla ya ligi kurejelewa tena katikati ya Januari mwakani.

Mwezi Mei mwaka 2014, watu walipoteza maisha baada mashabiki kupigana jijini Kinshasa wakati wa mchuano kati ya AS Vita Club na TP Mazembe.

Pamoja na hilo, inaonekana suala la siasa nchini humo limechangia mashabiki wanaoshabikia upinzani na serikali kuzozana kila wakati wanapokutana uwanjani.

Tahadhari hii pia imechukuliwa kuelekea tarehe 19, siku ambayo wapinzani wanamtaka rais Joseph Kabila aachie madaraka baada ya muhula wake kukamilika.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana