Pata taarifa kuu
UGANDA-SOKA

KCCA yaendeleza ushindi kutetea taji lake ligi nchini Uganda

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini Uganda KCCA, wamendeleza rekodi ya ushindi katika harakati za kutetea taji lake waliloshinda msimu uliopita.

Wachezaji wa klabu ya KCCA baada ya kupata ushindi siku ya Jumanne
Wachezaji wa klabu ya KCCA baada ya kupata ushindi siku ya Jumanne kccafc.co.ug
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, katika uwanja wa Lugogo jijini Kampala, mabingwa hao waliwaangusha Express FC mabao 3-1.

Muzamir Mutyaba, Geoffrey Sserunkuuma na Robert Ssentongo ndio walioipa klabu yao ushindi katika mchuano huo uliowakutanisha watani hao wa jadi walio na mashabiki wengi jijini Kampala.

 

KCCA ambayo inaogoza ligi kwa alama 18 itachuana na Vipers katika ujao katika uwanja wa Nakivubo katikati ya jijini Kampala.

Kikosi kilichocheza mechi hiyo: Benjamin Ochan, Timothy Awany, Habib Kavuma, Joseph Ochaya, Rukundo, Ivan Ntege, Isaac Kirabira, Muzamir Mutyaba, Paul Mucureezi, Robert Ssentongo, Brian Majwega.

Wachezaji wa akiba: Douglas Kisembo, Geoffrey Sserunkuma, Vicent Kayizzi, Tom Masiko, Denis Okot, Paul Musamali, Ronald Musana.

Katika mchuano mwingine, uliopigwa siku ya Jumanne, Vipers waliifunga Lwaza FC bao 1-0 katika uwanja wa Mutesa Wankulukuku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.