Pata taarifa kuu
SOKA-FIFA

Toure asikitishwa na uamuzi wa FIFA kuvunja tume muhimu

Kiungo wa Kati wa klabu ya soka ya Manchester City nchini Uingereza Yaya Toure, amesema amesikitishwa mno na uamuzi wa Shirikisho la soka duniani FIFA, kuvunja Tume maalum iliyoundwa kushughulikia suala la ubaguzi wa rangi katika mchezo wa soka.

Mshambuliaji wa klabu ya Manchetser City Yaya Touré
Mshambuliaji wa klabu ya Manchetser City Yaya Touré Reuters / Phil Noble
Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Ivory Coast, ambaye wiki iliyopita alitangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa, amesema uamuzi huo hauleti maana yeyote.

Toure ambaye alikuwa mmoja wa wadau katika Tume hiyo, amesema hatua hii ya FIFA huenda ikasababisha hali kuwa mbaya kuelekea kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

“Nimesikitishwa sana na uamuzi huu wa FIFA ,” alisema Toure baada ya kupokea barua ya kumpa taarifa hiyo.

Mchezaji huyu ameongeza kuwa hatua hii ya FIFA itawaumiza mashabiki wa wachezaji katika siku zijazo.

Mbali na Toure,wadau wengine wa mchezo wa soka wamekosoa hatua hii akiwemo aliyekuwa wakati mmoja naibu raia wa FIFA na Mwanamflame wa Jordan Ali bin Al Hussein.

FIFA kupitia Katibu wake Mkuu Fatma Samoura, imejitetea na kusema kuwa tume hiyo iliyoundwa mwaka 2013 imemaliza kazi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.